Kocha mkuu wa timu ya Kagera Sugar amesema wachezaji wake wamekuwa hawasikilizi maelekezo yake ndio sababu ya timu hiyo kuwa na mwenendo mbovu kwenye ligi.

Kagera ilikubali kipigo cha mabao 3-0 jana kutoka kwa Young Africans nakuifanya kuendelea kubaki nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ikilingana alama na Njombe Mji FC wanao buruza mkia.

Katika mchezo wa jana Kagera Sugar walicheza vizuri hasa kipindi cha kwanza kwa kutengeneza nafasi lakini walishindwa kuzitumia.

Mexime amesema wachezaji wake wamekosa umakini wakiwa uwanjani lakini anaendelea kuyafanyia kazi mapungufu yanajitokeza katika mechi zijazo.

“Wachezaji wanafanya makosa mengi ambayo yamekuwa yakitugharimu mara kwa mara lakini hatukati tamaa tutaendelea kupambana,” alisema kocha huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar.

Pogba apambana na hali yake, hatarini kuwakabili Liverpool
Maandamano yanayohamasishwa na Mange Kimambi ni uhaini