Kipa wa Yanga, Metacha Mnata amekiri kuwa na ugumu katika ushindani baina yake na makipa wenzake kwani mpaka sasa hana uhakika wa kuwa kipa namba moja licha ya kudaka mechi zote za kimataifa.

Metacha amesema mchuano dhidi yake na makipa wenzake, Farouk Shikalo raia wa Kenya na Ramadhani Kabwili kuwania namba moja ni mkubwa na anaona lolote linaweza kutokea muda wowote kwavile kila kipa ana uwezo na anaonyesha juhudi kubwa mazoezini.

Metacha alisajiliwa na Yanga msimu huu akitokea Mbao FC na tayari amedaka mechi zote za mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township na Zesco United.

“Unajua kila mchezaji anapambana na lengo ni kuwa bora na kuonekana na timu zile kubwa ndiyo maana unakuta mimi naweka bidii kwa kufanya vizuri kila ninapopata nafasi.

“Nataka kuwa bora na kuwa wa kimataifa ndiyo maana napambana kufikia malengo yangu japo ushindani ni mkubwa kama hapa tupo makipa wote wazuri na wenye uwezo lakini utapangwa kutokana na uwezo wako,”alisema Metacha.

Kipa huyo aliwahi kuibuka kipa bora wa michuano ya Sportpesa Super Cup ambayo ilifanyika hapa nchini mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Amuua baba, mama na kaka yake kisa mpenzi wa Twitter
LIVE: Rais Magufuli akipokea taarifa ya watuhumiwa 467 wa uhujumu uchumi wanaotubu