Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar ni majina matatu yaliyotajwa katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA kwa upande wa wanaume.

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo aliisadia klabu yake kushinda kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya pili mfurulizo huku akiibuka kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kupachika mabao 12.

Kwa upande wa Lionel Messi na Neymar waliisadia Barcelona kushinda kombe la Copa de Rey huku wakishindwa kuchukua kombe la ligi kuu ya Hispania La Liga.

Mlinda mlago wa Juventus Gianluigi Buffon ametajwa kuwania tuzo ya goli kipa bora wa kiume akichuana na kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer pamoja na Keylor Navas wa Real Madrid.

Kwa upande wa makocha, Zinedine Zidane, Antonio Conte na kocha wa klabu ya Juventus Massimiliano Allegri wametajwa kuwania tuzo ya kocha bora wa wanaume wa FIFA.

Antonio Conte alishinda ligi kuu ya Uingereza ‘EPL’ msimu uliopita

Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA upande wa wanawake itawaniwa na mshambuliaji wa Venezuela Deyna Castellanos, kiungo wa Marekani Carli Lloyd na Lieke Martens aliyesaidia Uhoranzi kushinda kombe la Euro 2017.

Tuzo hizo zitafanyika mjini mwezi Octoba jijini London Uingereza

 

Prof. Mbarawa anena kuhusu baraza la ujenzi NCC
Video: Mbowe apinga kuondolewa kwa Lissu Kenya, anena mazito