Ole Gunnar Solskjaer, ambaye ni meneja wa klabu ya Manchester United amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo baada ya kuchezea kichapo cha  4 bila toka timu ya Everton katika mchezo wa ligi kuu ya England.

” Nataka niombe radhi kwa mashabiki wote wa klabu hii tulizidiwa katika kila idara ila tulipata hamasa ya kutosha toka kwa mashabiki wetu na tutajitahidi kufanya vyema siku ya jumatano.” amesema Ole Gunnar Solskjaer.

Ole Gunnar Solskjaer amezungumza hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

“Ni ngumu kuweka katika maneno vile ninavyojisikia baada ya kipigo kikubwa toka Ole apewe jukumu la kuinoa klabu hiyo.” amesema goli kipa wa Man U De Gea.

United wamepoteza jumla ya michezo 6 ya hivi karibuni ikiwa ni michezo nane katika michuano yote waliyokuwa wakishiriki ikiwemo ligi ya mabingwa barani ulaya.

Mchezo dhidi ya Everton ulikuwa ni muhimu sana kwa klabu hiyo katika mbio za kuwania nafasi nne za juu ili kuweza kushiriki ligi ya mabingwa msimu ujao.

Manchester United watashuka dimbani tena siku ya Jumatano kuwakabili majirani zao Manchester City wanaouwania ubingwa kwa mara ya pili mfulizo.

Umoja wa Afrika waingilia kati maandamano Sudan
Bobi Wine, wafuasi wake wakamatwa tena Uganda