Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amesema ni muhimu kuzingatia ushauri wa wataalam na viongozi katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona.

Amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Tweeter ambapo amesema Corona haipaswi kupuuzwa kwani itasababisha watu kuumwa na wengine kuputeza maisha.

”Pamoja na tahadhari zote tunazozichukua, tatu ni za muhimu mno na zinaimbwa kote Duniani; Tunawe mikono, Tuepuke mikusanyiko na Tukae majumbani mwetu! Tutekekeze hayo na tuzingatie ushauri wa Wataalam na Viongozi wetu. Tukipuuza tutaumwa na wengine tutakufa! Tusipuuze!” ameandika membe

Ikumbukwe kuwa Italia ndiyo nchi iliyoathirika zaidi kwa vifo duniani na ugonjwa wa corona ambapo mpaka hivi sasa jumla ya watu 9,134 wamefariki kwa Corona ndani ya nchi hiyo.

Meya Iringa aondolewa madarakani
Uganda: Padri ajichimbia kaburi baada ya Corona kuua ndugu zake Italy

Comments

comments