Waziri Mkuu aliyejiuzuru na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amekutana na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Awamu ya Nne, Bernad Membe katika msiba wa mama mzazi wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jijini Dar es salaam.

Wawili hao walijitosa katika kinyang’anyiro cha kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuomba kupitishwa na chama hicho tawala kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Aidha, katika mchakato huo jina la Lowassa lilikatwa mapema huku Membe akiwa miongoni mwa wagombea watano waliopitishwa na Kamati Kuu ya CCM, Wakishindwa na John Magufuli aliyepeperusha vyema bendera ya chama hicho kwa kuibuka na ushindi.

Hata hivyo, Ruth Busondole, mama wa Askofu Gwajima amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84

Video: Tundu Lissu nimetolewa risasi nyingine mwilini, Wabunge 11 wasota kizimbani

Dkt. Kaberuka ampongeza Rais Magufuli kwa kazi anayoifanya
Dkt. Kigwangalla: Msipowakamata nawashtaki kwa JPM