Serikali imezipiga faini ya shilingi bilioni 19 ambazo ni sawa na dola za kimarekani 8,636, 363 meli 19 na kuzipa siku 14 meli hizo kukamilisha faini hiyo inayowakabiri kwa tuhuma za kukiuka masharti ya leseni zao na kufanya uvuvi haramu na uchafuzi mkubwa wa mazingira katika ukanda wa uchumi wa bahari kuu.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA), Hosea Mbilinyi amesema kila meli inatakiwa kulipa faini ya bilioni moja na amezitaja meli hizo kuwa ni Tai Hong no.2, Tai Hong no. 8, Tai Xiang no.5, Tai Xiang no.5, Tai Xiang no. 8, Tai Xiang no. 9, Tai Xiang no. 9, Tai Xiang no. 10, Tai Xiang no.7, Tai Xiang no 6, Tai Hong no 6, Tai Hong no .7, Xian Shiji no. 81, Xin Shiji no. 82, Xin Shiji no. 83, Xin Shiji no. 86, Xin Shiji no.76, Xin Shiji no. 76, Jian Shen no.1

Wakili wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Divisheni ya Mashtaka Makao Makuu Dar es Salaam ambaye ni Mkuu wa Dawati la Makosa ya Mazingira na Maliasili, Wankyo Simon amesema wamiliki wa meli hizo wasipolipa fedha hizo ndani ya muda uliotolewa na serikali, utaratibu wa kuwafikisha mahakamani utafanyika.

Aidha, Wankyo ameongezea kuwa mbali na hatua hizo za mahakama, pia serikali itawasiliana na nchi zilizotoa bendera kwa meli hizo ili kuzifutia usajili na kutoruhusiwa tena kufanya shughuli za uvuvi katika sehemu yeyote duniani.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema zimekiuka sheria hiyo kwa kutoripoti katika Bandari za Dar es Salaam, Zanzibar, Mtwara au Tanga kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kuondoka katika Bahari Kuu ya Tanzania na kusababisha Serikali kukosa mapato kwa kiasi kikubwa.

“Kwa kitendo hiki cha kukiuka masharti haya ya leseni zao maana yake wameshiriki uvuvi haramu, wamechafua mazingira kwa kiasi kikubwa wamefanya uvuvi holela na makosa mengine ya baharini vitendo hivi vimekuwa vilikosesha taifa mapato kwa kiasi kikubwa na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli haitakubali tena kuchezewa na kugeuzwa Tanzania kuwa shamba la bibi, kwa kila mmoja kuja na kuvua anavyotaka katika bahari yetu,” amesema Mpina.

Aliongeza kuwa serikali haiko tayari tena kufanya kazi na watu wanaovunja sheria za nchi na kwamba operesheni ya kuzisaka meli hizo itaendelea na zitaendelea kukamatwa kila siku kwani uhuru waliokuwa nao wa kuiba rasilimali hizo za taifa, haupo tena katika awamu ya tano.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo anayeshughulikia Uvuvi, Dk Yohana Budeba amesema Serikali haina mchezo katika jambo hili  na itaendelea kuchukua hatua kali kwa lengo la kulinda rasilimali za nchi ili ziweze kunufaisha Watanzania na taifa kwa ujumla.

Video: Zari atoboa siri rasmi kuachana na Diamond, amwanika vibaya "kukumbatiana na ma X kwenye public"
Lissu amtaka Jaji Mutungi ajitafakari