Rapa Meek Mill anayetumikia kifungo chake gerezani nchini Marekani amefunguka tena kwenye mahojiano aliyofanya na Rolling Stone hivi karibuni kuhusu maisha yake.

Rapa huyo amesema kuwa hatawaruhusu familia yake kumtembelea katika gereza hilo kwa sababu hataki wamuone akiwa katika muonekano alionao hivi sasa ambao amedai ni wa ajabu.

“Sitairuhusu familia yangu ije hapa. Kama wataniona na mandevu haya, nywele hizi… wajiuliza sana kama kweli sasa niko hivi na niko hapa? Kitu ambacho sitaki,” alisema.

Aidha, alisema kuwa ameshuhudia mengi ndani ya gereza hilo na kwamba uonevu dhidi ya watu weusi ni lazima auanike na kuupinga pindi tu atakapomaliza kifungo chake.

“Kuna ndugu zetu wamefungwa hapa ambao hawakufanya jambo lolote la kuwafanya wawe hapa. Ninataka kuuzungumzia huu mfumo na inachowafanyia watu weusi,” aliongeza.

Novemba mwaka jana, Jaji wa Pennsylvania alimhukumu kifungo cha miaka miwili hadi minne jela rapa huyo kwa kuvunja masharti ya kipindi cha uangalizi/matazamio (probation).

Q Chief afunguka kuhusu kuzimiwa MIC stejini
Rihanna awapa Snapchat hasara kubwa kwa tangazo la 'kumpiga kofi'