Rapa Meek Mill ameendelea na msimamo wake wa kumkataa Jaji wa Mahakama ya Juu ya Pennsylvania, Jaji Genece Brinkley.

Kwa mujibu wa madai ya timu ya Meek, Jaji huyo ameendelea kuvuka mipaka ya kazi yake na kufanya kazi za waendesha mashtaka na wakati mwingine kuingiza maslahi yake binafsi.

Mwanasheria wa rapa huyo amesema kuwa Jaji huyo anajiingiza kwenye maisha ya muziki ya mteja wake

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni akiwa gerezani, Meek alidai kuwa kuna watu wengi ndani ya gereza hilo ambao wamehukumiwa kifungo na Jaji huyo wakati hawana hatia.

“Kuna ndugu zangu humu ndani ambao wamefungwa na hawajafanya kitu chochote. Mimi nataka nizungumzie huu mfumo na inachokifanya kwa watu weusi,” alisema.

Kesi yake itasikilizwa tena Aprili 16 mwaka huu lakini Mahakama haijaonesha dalili za kumbadilisha Jaji huyo.

Marekani yaweka vikwazo Sudan Kusini
Sheria zambana Lissu kugombea Urais TLS