Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee amewashukuru Watanzania kwa maombi yao pindi alipokuwa akiugua, huku akiwajulisha hali yake inaendelea vizuri kwasasa.

Halima Mdee ameandika katika ukurasa wake wa kijamii, ambapo amesema kuwa sasa hivi amesharuhusiwa kutoka hospitali, hivyo yupo nyumbani kwake, na anendelea vizuri kiafya.

Mdee ameandika ‘Habari za asbh Wakuu. Kwa heshima kubwa, naomba niwashukuru wote kwa maombi na salamu za pole. Nimeshatoka Hospitali na afya yangu inaimarika kwa kasi ya ajabu, Sina cha kuwalipa kwa Upendo wenu mkuu, Mungu awasimamie na kuwabariki katika kila jambo mnalolifanya,’

Aidha, Jumamosi ya Juni 9, zilitolewa taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Joh Mrema, kuwa hali ya Halima Mdee haipo sawa kutokana na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kutolewa uvimbe tumboni.

Video: Mawaziri 7 ambao hawajaguswa na JPM, Utata wagubika kifo kigogo wa polisi
LIVE: Yanayojiri Bungeni jijini Dodoma leo Juni 10, 2019