Video vixen, Nascat Abdul maarufu kama Amber Ruty sambamba na Mpenzi wake, Saidi Bakari Kitomali hatimaye wamepata watu wa kuwatolea dhamana, juu ya kesi yao inayowakabili.

Dhamana hiyo imetolewa leo, Novemba 27 ambapo Amber Rutty amedhaminiwa na ndugu yake, huku mpenzi wake akidhaminiwa na Mchungaji Daudi Mashimo wa Kanisa la Emmaus Bible Church, Mbezi Luis DSM.

Aidha, hapo jana Hakimu Mkazi Mkuu Makama ya Kisutu, Augustine Rwezire alisema kuwa dhamana ya wawili hao bado iko wazi, ambapo ilikuwa ikihitaji wadhamini ambao kila mtu atasaini bondi ya Shilingi Milioni 15, wawe na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati za kusafiria, pia wasitoke nje ya Dar es Salaam bila ruksa.

Hata hivyo, ikumbukwe kwamba Mchungaji Daudi Mashimo ndiye aliyetangaza kufanya maombi maalumu kwa  Wema Sepetu, na kumtaka muigizaji huyo kuokoka ili kuondokana na mikosi inayomkabili katika maisha yake.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 28, 2018
Kawafundishe uzalendo unao waongoza, vinginevyo wataishia Gerezani- JPM