Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu 22 kwa matukio tofauti ambapo watatu kati yao akiwemo mchungaji wa Kanisa la Aglikana Shekandi Ashery Mkombola (44) wanatuhumiwa kukutwa na nyara za Serikali vipande18 vya meno ya Tembo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Gilles Muroto amesema watuhumiwa hao wa nyara za Serikali walikamatwa katika matukio mawili tofauti ambapo mchungaji huyo wa Kanisa la Kijiji cha Chinyika kilichopo Wilayani Mpwapwa amekutwa akisafirisha meno mawili ya Tembo yenye uzito wa kilogram 15.

Jafo: Muda wa kuchukua fomu hautaongezwa ” Msifunge ofisi”

“Mchungaji huyu alikamatwa katika Kijiji cha Pwaga kilichopo tarafa ya Kibakwe ingawa anaishi Kijiji cha Mungui na alikua akisafirisha meno hayo kwa kutumia pikipiki aina ya Fekon yenye namba za usajili MC 772 AYK,” amefafanua Muroto.

Amesema katika tukio la pili watuhumiwa wawili ambao majina yao yanahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi wamekamatwa katika stendi ya mabasi ya nanenane Jijini Dodoma wakiwa na vipande 16 vya meno ya Tembo wakitumia mbinu ya kuvificha katika dumu la lita 20 lililokatwa juu.

Rais Magufuli ampa ujumbe mzito CAG mpya, “Usibishane, kasafishe uchafu…”

Katika tukio jingine Kamanda Muroto amesema Polisi inawashikilia watu wawili Sam Ally Isihaka (44) dereva wa gari aina ya benz lenye namba za usajili AIB 5596 na Mwinyi Ramadhani Magumila (47) dereva wa gari aina ya benz lenye namba za usajili AIB 6924 kwa kosa la kukwepa ushuru.

Amesema watuhumiwa hao wakiwa safarini kutoka Malawi kuelekea Rwanda walikwepa ushuru wa Serikali katika mizani ya Uyole Mbeya, Makambako Njombe na Wenda Tanangozi Iringa kwa kushawishi na kutoa rushwa kwa maafisa wa mizani.

Ndugai afunguka CAG Kichere anavyotegemewa

“Maafisa hawa wa mizani nao walipokea rushwa na kutoa risiti bandia ili kuruhusu magari hayo mali ya kampuni ya Reginal Logistics ya Dar es salaam kupita bila kupima ambapo walikuwa wamezidisha uzito wa mizigo zaidi ya 650 gvm yaani gross vehicle mass,” amebainisha Kamanda Muroto.

Kufuatia tukio hilo Muroto amesema watuhumiwa sita wakiwemo maafisa wa mizani waliokuwa zamu katika vituo hivyo wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na wanatarajia kufikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Aidha katika tukio jingine Polisi inawashikilia watu kumi kwa makosa ya kuvunjwa na kuiba nyakati mbalimbali na kukutwa na mali za wizi flat screen TV 13, simu janja saba, home theater moja, laptop mbili, CPU moja na monitor moja.

Kamanda Muroto amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Amani Ally (26), Juma Said (22), Jumanne Ernest (21), Jafari Juma (25), Joseph Donald (30), Mena Ramadhani (52) na Rekresia Mchiwa (36) wote wakiwa ni wakazi wa Jijini Dodoma.

Hawa ndiyo viongozi wanaoapishwa na Rais Magufuli leo

” Yupo pia mtuhumiwa Fatma Mchiwa (35), Catherine Mtaturu (52) na Charles Mjema (52) hawa wote kwa pamoja wanatarajia kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili mara baada ya upelelezi kukamilika,” ameongeza Muroto.

Aidha katika tukio la mwisho Polisi inamshikilia Adema Massawe (44) kwa kukutwa na pombe haramu ya moshi lita 60 Novemba 3, 2019 katika eneo la maili mbili lililopo Jijini Dodoma na anatarajia kufikishwa Mhakamani.

Kufuatia matukio hayo Kamanda Muroto amesema jamii ikubali kubadilika kwa kufanya kazi halali ya kujiingizia kipato ili kuepuka uhalifu unaoweza kusababisha familizia zao kuteaeka kwa kukosa uangalizi kwani mwisho wa uhalifu ni majuto.

Vyama vya ushirika Singida vyahimizwa kukabiliana na wadudu
Jafo: Muda wa kuchukua fomu hautaongezwa " Msifunge ofisi"