Mataifa ya Nigeria, Namibia, Guinea-Bissau, Jamuhuri ya Afrika ya Kati na Malawi yameanza vyema harakati za kusaka nafasi ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON 2021), kwa kushinda, michezo yao ya nyumbani.

Wenyeji wa fainali za 2021, timu ya taifa ya Cameroon, wameshindwa kuanza vyema harakati hizo, kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya wageni kutoka visiwa vya Cape Verde, huku Lesotho wakilazimisha matokeo ya bao moja kwa moja dhidi ya Sierra Leone.

Timu ya taifa ya Nigeria, ililazimika kutoka nyuma kwa bao moja na kufanikisha ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Benin 2-1, katika mchezo wa kundi L.

Mkongwe Stephane Sessegnon aliifungia Benin bao la kuongoza dakika tatu baada ya kupyenga cha kwanza kupulizwa, akitumia makosa ya mlinda mlango wa Nigeria Daniel Akpeyi.

Dakika ya 40 Nigeria (The Super Eagles) walikaribia kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mchezaji wa Villareals Samuel Chukwueze, lakini shuti lake liligonga mwamba.

Hata hivyo dakika ya mwisho kabla ya kwenda mapumziko, wenyeji walifanikiwa kufunga bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati iliyopigwa na Victor Osimhen.

Mkwaju huo wa penati ulitokana na mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa anaitumikia Torino ya Italia Ola Aina, kuangushwa kwenye eneo la hatari.

Mshambuliaji wa Bordeaux ya Ufaransa Samuel Kalu, aliifungua Nigeria bao la ushindi dakika ya 60.

Kwa matokeo hayo Nigeria wanaongoza msimamo wa kundi L, Sierra Leone na Lesotho zinafuatia baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja huku Benin wakiburuza mkia wa kundi hilo.

Matokeo ya michezo mingine ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON 2021) iliyochezwa jana Jumatano.

Namibia 2-1 Chad (Kundi A)

Malawi 1-0 South Sudan (Kundi B)

Burkina Faso 0-0 Uganda (Kundi B)

Sudan 4-0 Sao Tome and Principe (Kundi C)

Angola 1-3 Gambia (Kundi D)

Jamuhuri ya Afrika ya kati 2-0 Burundi (Kundi E)

Cameroon 0-0 Cape Verde (Kundi F)

Guinea Bissau 3-0 Eswatini (Kundi I)

Senegal 2-0 Congo (Kundi I)

Nigeria 2-1 Benin (Kundi L)

Sierra Leone 1-1 Lesotho (Kundi L)

Wasio sajili laini kwa vidole kuendelea kupeta mwakani
Wazimia baada ya fedha za kikoba kuyeyuka kwenye kibubu