Wananchi wa Kijiji cha Mpanda Kata ya Nyimbili Wilayani Mbozi Mkoani Songwe wameshikwa na taharuki baada ya mbwa aliyewasumbua kwa siku nyingi kwa matukio ya uhalifu hasa kwa kukamata kuku kijijini hapo kugeuka na kuwa binadamu na kuanza kuongea.

Tukio hilo limethibitishwa na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho ambapo amesema kuwa wamekumbwa na taharuki kubwa kuona kitu cha ajabu binadamu kujibadilisha kuwa mbwa na kuanza kufanya uhalifu kitu ambacho kimewashitua wengi.

Aidha, inadaiwa kuwa mbwa huyo kwa siku alikuwa anakamata kuku kuanzia watatu mpaka wa tano, hivyo kuwafanya wananchi kuishi kwa hofu.

“Kuku walianza kupotea muda mrefu kitongoji cha Mpanda kati kwa hiyo baada ya hapo tumeamua kuamka na kuanza kufukuzana na huyo mbwa, tulianza kufukuzana naye kuanzia saa kumi na mbili na kufika saa nne ya asubuhi wakati tunakaribia kumkamata akabadilika na kutokea binadamu,”amesema Afisa Mtendaji.

Afisa Mtendaji huyo amesema kuwa baada ya mbwa yule kubadilika na kuwa binadamu alianza kuongea akiwaomba wananchi wasimrudishe kwao Ilemi bali wamuue na kukiri kuwa yeye ni mchawi na alitumwa.

“Nimekuja kuna mtu amenileta ila mama yangu ni mshirikina alichomewa nyumba kule Ilemi kwa hiyo mimi ni yule mbwa ambaye alipotea kule Ilemi aliyekuwa anatuhumiwa kwamba anakichaa, hivyo nikivaa tu hizi nguo nitabadilika kuwa mbwa yule wa Ilemi ambaye ni kichaa,”amesema Happy Victor

Hata hivyo, kwa upande wake Afisa Tarafa ya Vwawa, Haji Hamisi Ibrahamu amewataka wananchi kuachana na mambo ya kishirikina ambapo amewataka wazee wa mila na wachungaji wakemee tukio hilo na kusema kuwa mtu huyo watamfikisha kwenye vyombo vya sheria kwa kufanya uhalifu.

 

Alichosema Muliro juu ya majeruhi wa risasi tukio la maandamano ya Chadema
Video: Zari atoboa siri rasmi kuachana na Diamond, amwanika vibaya "kukumbatiana na ma X kwenye public"