Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Cosato Chumi amekabidhi Magari mawili kwa Idara ya Elimu Halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa lengo la kuongeza nguvu ya ufuatiliaji wa masuala ya elimu.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya Teachers Resource Centre (TRC Mafinga) wakati wa mkutano wa tathimini ya Elimu kwa Halmashauri ya Mji wa Mafinga ambapo umewakutanisha takribani waalimu wakuu wa shule zote za Sekondari na Msingi, Maafisa Elimu Kata, Wilaya na Wataalamu wengine wote wa Sekta ya Elimu.

Akizungumza na Wataalamu hao wa elimu, Cosato Chumi amesema kuwa elimu kwa wananchi ni muhimu sana katika jimbo lake na taifa kwa ujumla.

“Mimi naamini kwamba elimu ndio kila kitu bila elimu tusingekuwa hapa, kwa hiyo tunapokaa kufanya tathimini ya elimu tunapanga ili kuboresha elimu ya watoto wetu,”amesema Chumi

Aidha, amesema kuwa Halmashauri ya mji huo bado ni changa na ilianzishwa hivi karibuni, hivyo idara nyingi bado zina uhaba wa magari.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mufindi, Jamhuri William amempongeza mbunge huyo kwa kulipigania jimbo la Mafinga mjini katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwani amekuwa msaada mkubwa sana.

Tanzania yaalikwa maonyesho ya vipodozi China
Video: Tabasamu la Anthony Joshua lamkera Miller, nusura wazichape