Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoa wa Njombe, Neema Mgaya amehitimisha ziara ya kikazi Mkoani hapo kwa kugawa Mifuko 150 ya Saruji yenye thamani ya Tsh, 2,250,000/= ili kuunga Mkono nguvu za Wananchi katika shughuli mbalimbali za ujenzi.

Neema Mgaya amesema Saruji hiyo imegawanywa kulingana na Mahitaji husika na kupelekwa maeneo tofauti Mkoani Njombe ambayo ni Shule ya Sekondari Ludewa, Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu Ludewa na Shule ya Msingi Ushindi Kata ya Lyamkena Mjini Makambako.

Ametaja maeneo mengine kuwa kuchangia Ujenzi wa Zahanati Kata ya Utengule, Ujenzi wa Ofisi ya Kijiji Ngamanga, Zahanati ya Kanisa Katoliki Mtwango, Ujenzi wa  Kanisa Pentekoste Igwachanya, Shule ya Sekondari Usuka, Ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Kata Wanging’ombe, na Ujenzi wa Ofisi ya Serikali Kata ya Uhenga Wilayani humo.

Licha ya kutoa Saruji Mifuko 150 katika Mkoa wa Njombe, Mgaya amekabidhi Bendera 100 za Chama Cha Mapinduzi zilizogharimu kiasi cha Tsh, 300,000/= kwa ajili ya Mabalozi 100 wa CCM Mkoani hapo na kukabidhi Mafriji makubwa 15 kwa Wafanyabiashara wa Vinywaji baridi katika Maeneo tofauti Mkoani Njombe.

Akiwa katika Kata ya Utengule Mjini Makambako Neema Mgaya aliwatembelea Watu wenye uhitaji maalumu wakiwemo wanawake wajane na Watoto yatima wanaosaidiwa na Diwani wa Kata hiyo kisha kuwachangia Fedha kiasi cha Tsh, Lakimoja na kugawa Mahitaji yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Utengule, Stephano Mgoba (CCM).

“Nimeliza ziara yangu ya kikazi katika Mkoa wa Njombe na kufanikiwa kuchangia Vitu mbalimbali na Fedha tasilimu vilivyogharimu Jumla ya Fedha za kitanzania kiasi cha Tsh 2,650,000/=” Ameeleza, Neema Mgaya Mbunge wa Viti Maalumu, CCM Mkoa wa Njombe.

Wanafunzi wa mgambo wafariki kwa Adhabu mafunzoni
Video: Membe amshukia Kabudi kunaswa ndege yetu , Magufuli awaweka roho juu watendaji

Comments

comments