Baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kumfukuza bungeni Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Susan Kiwanga (CHADEMA) kwa kile alichodai ni utovu wa nidhamu, amefunguka na kudai kuwa hawezi kujibizana na kiti cha kiongozi huyo.

Spika Ndugai alifikia uamuzi huo baada ya kukaa kwa muda akitaka vyombo vimsaidie kumpata mbunge aliyefanya utovu wa nidhamu wakati mbunge wa Tandahimba (CUF) Katani Ahmed Katani alipokuwa akitoa mchango wake.

Katani alikuwa akikanusha madai ya kujiuzulu akisema vyombo vya habari havikumtendea haki ndipo wabunge wa upinzani wakaanza kupiga kelele lakini Spika alipowanyamazisha wakaanza kuzomea.

Akizungumza na Kiwanga amesema kuwa akiwa kama Mbunge mwenye jimbo, ana shughuli nyingi za kufanya jimboni kwake kuliko hata kuhudhuria vikao vya bunge, hivyo ameupokea uamuzi wa Spika Ndugai kwa mikono miwili.

“Wakati akichangia Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia (CCM), wenzake walikuwa wanashangilia kwakuwa alikuwa akitusema upinzani kuwa tunamzuia Katani kujiuzulu, na ndio maana wakati Katani akiongea na sisi tuliamua kumshangilia ndipo mgogoro ulianzia pale”, amesema Kiwanga

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 17, 2018
Diwani wa Chadema afikishwa Mahakamani