Hukumu juu ya maamuzi ya kupewa au kutopewa dhamana kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko imeonekana kuwa ngumu baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha ombi la kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa awali wa Mahakama Kuu.

Jamhuri imetangaza nia hiyo baada ya Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam, kutupilia mbali baadhi ya hoja zao kwa kile alichokieleza kukosa msingi wa kisheria.

Upande wa Jamhuri umewasilisha maombi ya kutosikilizwa kwa rufaa hiyo dhidi ya washtakiwa Mbowe na Matiko kwa kile walichokisema kuwa baadhi ya vipengele vya kisheria ambavyo vilitumika vinainyima sifa mahakama hiyo kusikiliza rufaa.

Kwa upande wa mawakili wa watuhumiwa Mbowe na Matiko walieleza kupinga taarifa hiyo ya rufaa kwa kile walichokidai kuwa upande wa jamhuri haujafuata baadhi ya taratibu za mahakama.

Mbowe na Matiko ni miongoni mwa viongozi saba, ambao wanakabiliwa na kesi ya msingi ya kusababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi Chuo Cha Usafirishaji cha NIT,  Akwilina Akwilini pamoja na makosa mengine ya uchochezi.

Mbali na viongozi hao, viongozi wengine wanaoshtakiwa kwenye kesi hiyo ya msingi ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt Vicent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu, pamoja na Mbunge wa Kibamba John Mnyika

Jela miaka 20 kwakukutwa na kucha za Simba
Serikali kuzifanyia mapitio upya Leseni za uchimbaji madini