Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa Mkoa wa Kilimanjaro hautegemei maendeleo kutoka Chama cha Mapinduzi CCM.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa  Machame Uroki katika ziara yake ya kutembelea jimboni mwake.

Amesema kuwa Kilimanjaro imeendelea kutokana na wazee wa miaka iliyopita kupata elimu ya kutosha ambayo imekuwa chachu ya maendeleo mkoani humo.

“Sifa kubwa kuhusu mkoa wa Kilimanjaro ni elimu, wazee wetu walikuwa wasomi sana kuliko mikoa mingine, kwa hiyo maendeleo ya Kilimanjaro hayategemei CCM, yalikuwepo hata kabla ya uhuru, watu wa Kilimanjaro walisoma siku nyingi,”amesema Mbowe.

Aidha, Mbowe amewataka wananchi kuwekeza katika elimu kwani ardhi ya kuwarisisha watotho kwa sasa haipo Kilimanjaro.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wananchi wa mkoa huo wanatakiwa kujikita zadi katika kuwekeza kwene elimu ili waweze kuendana na soko la ushindani.

Wakulima wa mazao yaliyo sahaulika kuneemeka
Polisi wamshikilia mbunge wa CCM