Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amekanusha taarifa alizotoa mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Siha, Dkt. Mollel kuwa aliamua kuhama CHADEMA kwenda CCM kwa kuwa alizuiwa kuongea na viongozi wa chama hicho.

Ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampeni za mgombea Ubunge wa CHADEMA katika jimbo la Siha, Elvis Mosi na kudai kuwa Dkt. Mollel hakuwa na uwezo wa kujenga hoja na ni mtu ambaye amekuwa akijikomba kwa watu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Huu ni mpango wa Mungu aliona wananchi wa Siha nikiwaachia hili gunia la misumari litakuwa si jambo zuri hivyo akamtia uchizi akaamua kuhama chama, kwa hiyo hatuna cha kulia kila kitu ni mpango wa Mungu, alijua kwamba Siha tumejitwisha gunia la misumari,”amesema Mbowe

Hata hivyo, Mbowe amesisitiza kuwa kitendo cha Dkt. Mollel kujivua uanachama na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge jimbo la Siha ni mpango wa Mungu na ni jambo zuri kwani lingefanya chama hicho kuchukiwa na wananchi.

 

Rick Ross ana bifu na Diamond? Amfuta Instagram
Magazeti ya Tanzania leo Januari 27, 2018