Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amejiweka karantini siku chache baada ya kutangaza kuwa mwanaye Dudley amepata maambukizi ya virusi vya Corona.
Mbowe amesema amejitenga na familia yake ambayo itakuwa karantini kwa wiki mbili, na hivi sasa yupo nyumbani Dodoma akisubiri majibu ya vipimo ili kufahamu kama ameambukizwa Virusi hivyo.

Amesema tangu aonane na Dudley siku 12 zilizopita, amekutana na watu wengi hivyo ni jambo la kuomba Mungu asikutwe na corona ili aliokutana nao pia wawe salama.

Aidha, Mbowe ameeleza kuwa mkakati wa pamoja unahitajika ili kukabiliana na mlipuko wa Corona ambao amesema ni suala ya kitaifa.

CORONA: RFEF kuzisaidia klabu zenye hali mbaya kiuchumi
Brg. Jenerali wa Takukuru apandishwa Cheo kwa kuokoa mamilioni