Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally amepokea madiwani 11 huku akibainisha Madiwani hao, 10 ni Madiwani wa Kuchaguliwa na Mmoja ni wa Viti Maalumu huku timu hiyo inayoongozwa na Meya ikiwa na Viongozi Watatu wa Juu wa CHADEMA.

Amesema kuwa Madiwani hao wanatoka katika Jiji la Mbeya kwenye Halmashauri inayoongozwa na CHADEMA na Mbunge wa Jimbo hilo ni Joseph Mbilinyi (Sugu) hivyo huo ni ugeni mkubwa tangu aanze kupokea Wageni.

Aidha, amesema ameongea na Madiwani hao na kumueleza kwanini wanafanya uamuzi huo wakati huo na amefurahi sana maana kazi yake ni kuifanya CCM kutoa ushawishi na kupata wafuasi kila kona ya Nchi.

Bofya hapa kutazama mapigo kumi ya CCM kwa upinzani kabla ya uchaguzi mkuu

Ukerewe: Uhaba wa Samaki, wananchi watakiwa kufuga nyuki
Kabendera aachiwa huru, apunguza faini milioni 100

Comments

comments