Mfamasia wa hospitali ya Wilaya ya Rungwe mkoni Mbeya amekuwa akianika kondomu juani kwa madai kuwa anataka kuzirejesha katika hali yake ya kawaida baada ya kubaini zinaharibika.

Hayo yameibuka baada ya ziara ya kushtukiza ya Naibu waziri wa afya, Faustine Ndugulile  katika hospitali hiyo amabpo amesema ni kosa kuhifadhi kondomu kwa mtindo huo kwa kuwa zinaharibika na hata kuwa chanzo cha maambukizi ya Virusi vya ukimwi (VVU) mkoani humo.

Naibu waziri huyo amesema kuwa ameamua kufanya ziara ya kustukiza hospitalini hapo baada ya kupata taarifa za siri kuwa kuna mambo yanafanyika kinyume na taratibu.

Akiwa katika chumba cha dawa Ndugulile alibaini baadhi ya baadhi ya nyaraka zinzaonyesha kuna dawa 50 ndani ya chumba hicho lakini alipohesabu alibaini ziko 30 huku baadhi ya dawa zilizotolewa haielezwi zilipopelekwa.

Aidha  Naibu waziri ameamuru Jeshi la Polisi kuwakamata watumishi wawili wa hospitali hiyo Vumilia Mwaijande, na mfamasia Elia Kandonga kwa tuhuma za kufanya ‘madudu’ ukiwemo wizi wa dawa na utunzaji mbovu wa baadhi ya dawa na vifaa tiba.

”Nakuagiza Mganga mkuu wa mkoa uunde timu ije hapa ichunguze mtiririko wa uingizwaji na utolewaji wa dawa katika hospitali hii kwa kipindi cha mwaka mzima, maana hapa inaonekana kuna wizi wa dawa za serikali” ameagiza Ndugulile.

Pia amemtaka mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya, Dkt. Salumu Manyata kumuondoa mara moja Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Manase Ngogo kwa usimamizi mbovu wa hospitali.

Naye katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe, Mnkondo Bendera amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo itashauriana ili kuchukua hatua stahiki kwa yeyote aliyehusika na uzembe katika hospiali hiyo.

Wizi wa betri za taa barabarani waibuka Moshi
Barrick kupunguza wafanyakazi zaidi ya 100 North Mara