Mbunge wa Vunjo kupitia NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema kuwa alikwenda kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kumueleza malalamiko yake juu ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba kwa madai ya kusitisha ujenzi wa barabara na kupelekea hasara ya mabilioni.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo lake Kata ya Makuyuni katika mamlaka ya mji mdogo wa Himo, wilaya ya Moshi wakati wa Mkutano wa hadhara baina ya kiongozi huyo na wananchi.

“Sasa tuone ni nani zaidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na maendeleo ya Watanzania, maendeleo hayana itikadi za vyama. Kwa nini amefanya hivyo, kwa sababu Jimbo la Vunjo tumekuwa wa kwanza Tanzania kuweza kujipanga wenyewe mpaka hatua tuliyofikia ya kujiletea maendeleo yetu wenyewe.”amesema Mbatia

Aidha, mradi wa upanuzi na ujenzi barabara za vijijini kwa kiwango cha changarawe unaodaiwa kusitishwa katika Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, unahusisha barabara zenye urefu wa kilometa 389.3 ambazo zilikuwa zigharimu Sh. bilioni 12.077 kutokana na utafiti wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(Tarura).

Hata hivyo, novemba 15 mwaka huu kupitia wakili wa kujitegemea, Harlod Sungusia alizungumza na waandishi wa habari juu ya madai ya kumshtaki Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba kwa madai ya kudaiwa fidia ya zaidi bilioni 2.

Anyongwa kwa sweta la mumewe
Unatafuta ajira? hizi hapa nafasi 10 za ajira kwa ajili yako