Mfanyabiashara wa madini ambaye ni raia wa China amejikuta akitiwa mbaroni na Takukuru kwa tuhuma za kumshawishi na kujaribu kutoa rushwa ya Sh nilioni moja na pakiti ya majani ya chai kwa Mkuu wa mkoa wa Geita, Robert Gabriel.

Mfanyabishara huyo amejulikana kwajina la Cheng Li, tayari ameburuzwa mahakamani kujibu tuhuma za kutaka kumpa rushwa kiongozi wa serikali wa mkoa wa Geita.

Hati ya mashtaka ilipokuwa inasomwa na mwendesha mashtaka wa Takukuru Denis Lekayo, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Jovith Kato, alieleza kuwa katika kipindi ya Oktoba na Novemba 10 mwaka huu mshtakiwa alimshawishi mkuu huyo wa mkoa kwanjia ya ujumbe wa simu kumpatia shilingi milioni moja kila mwezi.

Aidha mshtakiwa kwa kuonyesha amedhamiria kutoa rushwa alituma tena ujumbe kumshawishi kiongozi huyo apokee kiasi hicho cha fedha na paketi ya majini ya chai kutoka China, Baada ya kupata ujumbe huo,mkuu huyo wa mkoa alitoa taarifa Takukuru ambao waliweka mtego uliofanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa katika ofisi za mkuu wa mkoa  akiwa na shilingi milioni moja  pamoja na paketi ya majani ya chai.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 20, huku mshatakiwa akiwa amekana makosa yote na yuko nje kwa dhamana ya wadhamini wawili waliosaini bondi ya shilingi milioni mbili kila mmoja na kutakiwa kukabidhi hatiyake ya kusafiria.

 

Mgogoro wa Burundi na Rwanda wazidi kufukuta
Mfahamu Wilhelm Bleek aliye linganisha sarufi za Kibantu na kuziunganisha