Mshambuliaji kinda wa mabingwa wa soka nchini Ufaransa AS Monaco Kylian Mbappe, ameendelea kuwa sehemu ya kufikiriwa na rais wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid Florentino Perez,  katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.

Perez amekua mshawishi mkubwa kwa meneja wa kikosi cha Real Madrid Zinedine Zidane, ili akubali mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo ambaye pia anawani na matajiri wa jijini Paris PSG.

Msisitizo wa kiongozi huyo wa juu wa Real Madrid unadaiwa kupamba moto, kufuatia taarifa kutoka nchini Ufaransa kueleza kuwa, PSG wamekubali kutoa kiasi cha Euro milioni 180 kama ada ya uhamisho wa Mbappe kutoka AS Monaco.

Hata hivyo Diario Sport wameeleza kuwa, pamoja na uwepo wa makubaliano hayo,bado Mbappe anaonyesha nia ya kutaka kucheza soka nje ya Ufaransa, na chaguo lake kwa sasa ni kujiunga na Real Madrid.

Zidane amekua mzito kutoa maamuzi ya kusajiliwa kwa Mbappe, kutokana na uhusiano mzuri uliopo katika safu yake ya ushambuliaji ambayo inaundwa na Karim Benzema, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo.

Endapo atabariki dili la kusajiliwa kwa Mbappe, meneja huyo kutoka Ufaransa atalazimika kumruhusu Benzema ama Bale kuondoka klabuni hapo, kutokana na ufunyu wa nafasi kwenye kikosi cha kwanza utakaokuwepo.

Raila ahudhuria utangazaji wa matokeo akiwa na kitendawili
Zlatan Ibrahimovic Kurudishwa Old Trafford?