Bondia Floyd Maywether atapanda tena ulingoni mwezi Septemba 12 mwaka huu kuzipiga na Andre Berto.

Floyd atajaribu kuifikia rekodi ya bondia Rocky Marciano, ya kupigana mapambano 49 pasipo kupoteza.

Berto ameshinda mapambano 30 huku akipoteza mapambano matatu.

Uamuzi wa Mayweather unazima matumaini ya bondia mwingereza, Amir Khan aliyetamani mpango wake wa kupigana na bondia huyo utimie hasa baada ya kumpiga Chris Al mwezi Juni mwaka huu.

Mayweather alieleza kuwa baada ya pambano lake na Manny Pacquiao k atacheza pambano moja tu la mwisho kabla ya kustaafu mchezo wa masubwi.

Taarifa hii kutoka kwa timu ya Mayweather inafifisha matumaini ya wapenzi wa ndondi duniani kushuhudia pambano la marudiano kati ya bondia huyo na Manny Pacquiao.

Sunday Oliseh Kuanza Kazi Kwa Vitendo Dhidi Ya Taifa Stars
Waziri Mwingine Wa Kikwete Aanguka