Bingwa wa zamani wa masumbwi aliyeweka rekodi ya kutopigwa, Floyd Mayweather ameibua mijadala kwa wajuzi wa michezo ya mapigano, baada ya kutangaza mpango wa kushiriki mapigano ya ngumi na mateke ya UFC/MMA.

Mtangazaji maarufu wa mchezo wa masumbwi ambaye ni mjuzi wa michezo hiyo pia, Jim Gray amewataka wapenzi wa michezo hiyo kutojaribu kuweka sarafu yao dhidi ya Mayweather atakapoamua kuingia kwenye mchezo huo.

Amesema Mayweather sio wa ‘kumchukulia poa’ katika lolote kwani ameweza kushinda mapambano yake yote 50, rekodi ambayo ni ya kipekee.

“Usijaribu hata kidogo kuweka sarafu yako dhidi ya Mayweather. Ni mshindi mara 50 bila kupigwa (50-0),” TMZ inamkariri Gray.

Hata hivyo, bingwa wa mapigano ya UFC, Max Holloway amepingana na Gray akidai kuwa anachofanya Mayweather hivi sasa ni kutafuta kiki tu kwani hawezi kusimama na kupambana na wababe wa MMA tena wenye damu change zaidi yake.

Mayweather ambaye aliuza jina lake zaidi baada ya kumpiga mbabe wa UFC/MMA, Conor McGregory kwenye ulingo wa masumbwi, amedai kuwa na mpango wa kushiriki mapambano hayo miezi kadhaa ijayo.

Boko Haram wamng’ang’ania msichana mmoja kwa udini
Video: DataVision yatoa maelfu ya ajira, yaibua vipaji