Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) pamoja na vyama vingine kikiwemo chama cha mawikili Afrika mashariki mkoani Njombe wameiomba serikali kusogeza mahakama kuu mkoani humo pamoja na kuongeza idadi ya watumishi wa mahakama ili kukabiliana na idadi ya ongezeko kubwa la mashauri mahakamani.

Ombi hilo limetolewa na mawakili hao kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka wakati wa kilele cha wiki ya sheria iliyofanyika katika mahakama ya wilaya ya Njombe.

“ili kuboresha suala la utoaji wa haki kwa wakati tungependa kupendekeza ongezeko la idadi ya watumishi wa mahakama yaani majaji na mahakimu ili kukabiliana na ongezeko kubwa la idadi ya mashauri mahakamani ambapo waliopo kwasasa wamekuwa wakilemewa na mzigo mkubwa wa kazi, hivyo kufanya haki isitolewa kwa wakati,”amesema Wakili Tunsumwe

Amesma kuwa kilio kikubwa cha wananchi ni ucheleweshaji wa utoaji haki, kukosekana au uhaba wa vitendea kazi, miundombinu mibovu na umbali wa huduma ya mahakama. kuruhusu watu wasio na taaluma ya sheria kuaanda nyaraka za kisheria ambazo zimekuwa hazina ubora.

Kwa upande wake hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Njombe, Magdalena Nanson Mtandu amesema kuwa pamoja na mafanikio makubwa yanayotokana na chombo hicho cha mahakama, bado wameendelea kuboresha huduma za kimahakama ili kuweza kutoa haki kwa wakati.

Naye Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka ameahidi kufikisha maombi hayo kwa Rais ili kuona namna ya kuyatekeleza ili kuweza kuondoa usumbufu unaojitokeza kwasasa.

 

Nape aweka wazi sababu ya kujiuzulu uenyekiti Kamati ya Bunge
UVCCM Njombe kuitisha mkutano wa vijana kuhusu sakata la mauaji