Mkuu wa wilaya ya Njombe, Luth Msafiri amezindua rasmi msimu mpya wa kilimo 2019/2020 katika halmashauri ya mji wa Njombe akiwataka wakulima kuhakikisha wanapima udongo ili kuongeza mavuno zaidi.

Uzinduzi huo umefanyika Oct 11,2019 katika kijiji na kata ya Uwemba ambapo uliambatana na maonyesho ya pembejeo za kilimo kutoka kwa wadau wa sekta ya kilimo mjini humo.

Pamoja na mambo mengine, Msafiri amewaonya mawakala wa Pembejeo za kilimo wenye tabia ya kuwauzia wakulima pembejeo feki na wale wanaopandisha bei kiholela.

Amesema kuwa hatawavumilia wafanyabiashara wote wa pembejeo za kilimo wanaojihusisha na vitendo vya dhuluma kwa wakulima kwa kuwauzia pembejeo feki hususani mbegu za mazao mbalimbali.

Maonyesho hayo yalibeba kauli mbiu inayohamasisha wakulima wote kuwa na utaratibu wa kupima udongo kabla kupanda mazao yao Shambani kwa lengo la kuongeza Uzalishaji.

Uzinduzi kama huo umefanyika katika Halmashauri zote za Wilaya ya Njombe.

Waziri Hasunga akerwa kasi ya ujenzi wa Vihenge
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 13, 2019