Cecil Mwambe, aliyekuwa Mbunge wa Ndanda kupitia tiketi ya CHADEMA ametangaza kujivua uanachama pamoja na nafasi ya ubunge jimboni humo leo Februari 15, 2020.

Mwanasiasa huyo ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kanda ya kusini CHADEMA katika sababu alizozitoa, moja ni kuvumilia kwa muda mrefu matusi ambayo amekuwa anatukanwa yeye pamoja na familia yake bila chama hicho kuchukua hatua yeyote.

“Niliitwa majina yote mabayo mnayoyajua, lakini nilivumilia nikiwa najua na matusi yote yaliyotukanwa, mbaya zaidi mimi ni mwenyekiti wa Chama, vipi kwa mwanachama wa kawaida?” amesema Mwambe alipotoa taarifa yake kwenye ofisi ndogo za CCM Dar es salaam.

Licha ya kujiunga na CCM, Mwambe ameomba ridhaa ya kugombea tena ubunge ili kuwakilisha wananchi wa jimbo la Ndada, kwani safari ya kujenga upinzani wa kweli Tanzania bado ni ndefu na hajaridhika nayo.

” Kwakutumia haki yangu ya kikatiba nimeamua mwenyewe kujiunga na chama cha Mapinduzi na ninawaomba kama mtanipokea leo nipewe tena nafasi ya kugombea” Amesema Mwambe.

Akimpokea mwanasiasa huyo, Katibu wa itikadi wa uenezi CCM Humphrey Polepole amempongeza kwa uamuzi aliochukua na kusema bado hajaona vyama vya upinzani ambayo vipo tayari kutengeneza taasisi imara.

Maambukizi mapya ya virusi vya Corona yapungua
Kisiwa chote cha Zanzibar kupuliziwa dawa ya Malaria