Msanii wa Bongo Flava, Matonya amedhamiria kufikisha kilio chake kwa Rais John Magufuli kuhusu uhaba wa fedha mifukoni akitumia kipaji chake.

Matonya amekaririwa akieleza kuwa ataachia wimbo mpya alioupa jina la ‘Magufuli Legeza Kidogo’ ambao pia utatambulisha rasmi kundi lake jipya la ‘Black Image’.

“Kuna wimbo unakuja unaitwa ‘Legeza Kidogo’ au ‘Mr Magufuli Legeza Kidogo’, ni kazi ya vijana wangu ambao walikuwa wananisumbua kwa muda mrefu niwasaidie, kwa hiyo mimi ni kiongozi,” alisema Matonya.

Akizungumzia maudhui ya wimbo huo, Matonya alieleza kuwa umetokana na kilio cha uhaba wa fedha kwa wananchi, hivyo pamoja na kutambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Rais John Magufuli, anafahamu kwenye suala la upatikanaji wa pesa ‘hali sio shwari’.

Wimbo huo unaweza kuwakumbusha mashabiki wa bongo flava kuhusu wimbo wa ‘Ridhiwani’ ulioimbwa na Izzo Bizness akimuomba mtoto wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete afikishe ujumbe kwa Baba kuhusu ugumu wa maisha mtaani.

credit: Nipashe

Chadema wamtumbua Diwani wao kwa ufisadi
Video: Jaji Chande auzungumzia Mpango Mkakati wa Mahakama Tanzania