Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imesema ni mapema sana na ni kinyume cha sheria kwa mgombea wa upinzani, Raila Odinga kujitangazia kuwa ameshinda uchaguzi wa Kenya.

Aidha, muungano wa upinzani wa NASA umesema kuwa matoke yanaonyesha kuwa Raila Odinga amemshinda Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, pia wameitaka tume ya uchaguzi kumtangaza Odinga kuwa ndiye Rais mteule.

Matokeo hayo ya awali yaliyotangazwa na tume hiyo yanaonyesha Rais wa sasa Uhuru Kenyatta bado anaongoza dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga.

Hata hivyo, muungano wa NASA umepinga matokeo hayo ukisema kuwa yamechakachuliwa hivyo wameitaka tume hiyo kumtangaza Odinga kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya urais wa nchi hiyo.

 

Trump amshukuru Putin kwa kuwafukuza Wamarekani Urusi
Video: Watu 13 wauawa Kibiti, Bill Gates amwaga mabilioni Tanzania