Kiungo Mateo Kovacic amegoma kufanya mazoezi na kikosi cha Real Madrid kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini Hispania, kwa shinikizo la kutaka afahamishwe kuhusu mustakabali wake klabuni hapo.

Tangu jana Jumatatu, kiungo huyo ambaye alikua sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Croatia kilichofika hatua ya fainali, kwenye michuano ya kombe la dunia, amegoma kufanya mazoezi, akiamini maamuzi hayo yatamuweka katika hatua nzuri ya kujua kama ataondoka klabuni hapo, ama kuhakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza msimu ujao.

Mpaka sasa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, hajaambiliwa lolote na uongozi wa Real Madrid tangu alipoanza kuomba utaratibu wa kuuzwa katika kipindi hiki cha dirisha la usajili wa majira ya kiangazi, kufautia kuchoshwa na hatua ya kuwekwa benchi.

Kovacic, amewahi kuweka wazi hitaji la kutaka kuuzwa kipindi hiki, na anaamini kama jambo hilo litafanyika atakuwa na kila sanbabu ya kucheza mara kwa mara katika klabu itakayomsajili.

Tangu aliposajiliwa klabuni hapo mwaka 2015, Kovacic ameshakitumikia kikosi cha Real Madrid katika michezo 73 na kufunga bao moja.

Makonda aishika mkono TFF, sasa kuandaa AFCON U17 kwa pamoja
Willian afunguka ukaribu wake na Jose Mourinho