Wadau na mashabiki wa klabu ya Mbao FC mkoani Mwanza wameutaka uongozi wa klabu hiyo kujitathmini na kuzipitia upya changamoto zinazoikabili timu yao ikiwa ni pamoja na kumaliza migogoro ya ndani ili kuinusuru na kushuka daraja.

Kilio hicho kimetoka muda mfupi baada ya klabu hiyo kurejea jijini Mwanza ikitokea Dar es saalam ambako ilikubali kichapo cha bao 2-1 dhidi ya Azam FC ikiwa ni mfufulizo wa kupoteza michezo yake ya ugenini.

Katika mapokezi hayo baadhi ya wadau wa soka mkoani Mwanza wameunyooshea kidole uongozi wa klabu hiyo, kuhusika katika matokeo hayo, lakini Mwenyekiti wa klabu hiyo Sole Njashi ametupilia mbali baadhi ya malalamiko ya wadau hao.

Naye Katibu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza (MZFA) Leonard Malongo amesema njia pekee itakayoinusuru klabu hiyo ni mazungumzo ya mezani.

Mbao FC imerejea jijini Mwanza ikiwa na alama 19 ikishindwa kupata matokeo kaika michezo minne mfululizo ikiwa ugenini na hivyo kushika nafasi tatu kutoa mkiani ikitanguliwa na Njombe Mji yenye alama 18 na Majimaji inayoburuza mkia ikiwa na lama 15.

Liverpool kukutana uso kwa macho na Man City
Klopp akanusha tetesi za kuvunja rekodi ya Wenger