Mshambuliaji Mario Mandzukic ametangaza kuachana na timu ya taifa ya Croatia na kuelekeza nguvu zake katika upande wa klabu Juventus anayoitumikia kwa sasa.

Mshambuliaji huyo ametanagaza kustaafu kucheza timu ya taifa huku akikumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa wakati wa fainali za kombe la dunia 2018, na kufanikisha lengo la kuipeleka fainali Croatia.

Katika mchezo huo Mandzukic alifunga moja ya mabao ya kufutia machozi kwa timu yeke ya Croatia dhidi ya Ufaransa waliochomoza na ushindi wa mabao manne kwa mawili.

Katika fainali hizo ziliofanyika nchini urusi kuanzia Juni 14 hadi Julai 15, Mandzukic alifunga mabao matatu.

Mandzukic mwenye umri wa miaka 32, anaondoka kwenye kikosi cha Croatia akiwa amefunga mabao 33, akiachwa kwa mabao mawili na gwiji wa soka wa nchi hiyo Davor Suker. Ameitumikia timu hiyo katika michezo 89 tangu alipoitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2007.

“Imenilazimu kutangaza kustaafu soka la kimataifa, ni muda muafaka kwangu kufanya maamuzi haya, nimetoa mchango wangu kwa kiasi ninachoamini kinachosha,” Alisema Mandzukic alipohojiwa na mwandishi wa tovuti ya timu ya taifa ya Croatia.

“Nilijitoa kwa hali zote ili nifanikishe malengo kwa taifa langu, nimejitahidi kwa uwezo wangu, ninaamini vijana wanaokuja baada yangu watafanikisha makubwa ziadi na kuiwezesha timu yetu kufanya vizuri kimataifa siku za usoni,’

“Ninawashukuru mashabiki wa soka nchini Croatia na kwingineko duniani wanaoipenda na kuifuatilia timu yetu kila inapokua uwanjani, wao ni sehemu y amafanikio tuliyoyapata wakati wa faianli za kombe la dunia, ninaamini walichochea mafanikio niliyoyapata nikiwa na timu hii kwa wakati wote.”

Mbali na fainali za kombe la dunia, Mandzukic pia amewahi kuiwakilisha Croatia katika fainali za mataifa ya barani Ulaya, na aliwahi kutajwa kama mchezaji bora wa nchi hiyo kwa mwaka 2012 na 2013.

UN yampongeza Rais Kabila, yahimiza uchaguzi wa amani na haki DRC
Ligi ya mabingwa Ulaya 2018/19