Mwanaharakati na muasisi wa harakati ya Change Tanzania, Maria Sarungi ameonesha kushangazwa na taarifa za Chadema alizodai zimemtaja kuwa alinunuliwa na CCM kusaidia kufikisha matokeo ya utafiti wa Twaweza uliompa ushindi Mgombea urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli kwa asilimia 65 dhidi ya Edward Lowassa wa Chadema.
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Maria Sarungi ambaye hivi sasa amekuwa akikutana na changamoto kubwa ya jumbe zinazomkosoa zinazoaminika kuwa zinatoka kwa watu wanaounga mkono Ukawa, alisikitishwa na jinsi ambavyo akaunti inayoaminika kuwa rasmi ya Chadema ilivyodai amenunuliwa.
So officially @ChademaMedia inadai kuwa mimi nimenunuliwa? Let me get confirmation. https://t.co/n2jny7yhoT
— Maria Sarungi Tsehai (@MariaSTsehai) September 25, 2015
Saa kadhaa baada ya Twaweza kutoa matokeo ya utafiti wao, picha kadhaa zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha Maria Sarungi akiwa na wafanyakazi wa Twaweza na makada wa CCM akiwemo Mwigulu Nchemba.
Hata hivyo, picha hizo zilidhihirika baadaye kuwa zilikuwa zamani na zilichukuliwa katika moja kati ya tukio la maandalizi ya mahojiano kati ya Maria Sarungi na Mwigulu Nchemba.
Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Twitter wamekuwa wakimtaja mwanaharakati huyo kama mmoja katia ya wafanyakazi wa Twaweza kitu ambacho amekuwa akikipinga kwani yeye ni mratibu wa midahalo ya Mkikimiki na sio vingenevyo.
Thank you @TheCitizenTZ for clearing up. Hii picha ya juzi nilivaaje na nilialikwa kutoa maoni si mwajiriwa ? pic.twitter.com/mlqF7GzVJB
— Maria Sarungi Tsehai (@MariaSTsehai) September 24, 2015