Serikali ya Marekani imeongeza vikwazo vingine kwa Korea Kaskazini ikiwa ni hatua ya kwanza tangu mkutano kati ya Rais Donald Trump na Kim Jong Un kuvunjika.

Marekani imeyaadhibu makampuni mawili ya Kichina yanayodaiwa kuisaidia Korea Kaskazini kuvunja masharti ya vikwazo vilivyowekwa na nchi hiyo pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Afisa mwandamizi wa Marekani aliiambia CNN kuwa hatua hizo hazipaswi kuonekana kama mpango wa Marekani kuharibu mfumo wa kiuchumi wa Korea Kaskazini bali ni katika kuhakikisha kuwa nchi zote pamoja na makampuni haziendi kinyume na masharti yaliyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

“Hii ina maanisha kuwa ni shughuli endelevu ya Marekani na nchi nyingine kuhakikisha tunazingatia uadilifu katika vikwazo vilivyowekwa,” CNN inamkariri afisa huyo ambaye hakutajwa jina.

Kwa mujibu wa Rais Trump, katika mkutano wa Honai kati yake ya Kim Jong Un, Korea Kaskazini ilitaka vikwazo vyote vikuu viondolewe kama sehemu ya hatua ya wao pia kuachana na mpango wa makombora ya kinyuklia.

Korea Kaskazini imeeleza kuwa Marekani ilipoteza nafasi ya dhahabu katika mazungumzo hayo na kwamba hawategemei kuwa wataifapa tena na hawataombwa kufanya hivyo.

Kwasasa hatuhitaji kuungwa mkono na mbunge yeyote- CUF
CUF yaelezea itakavyorudisha ‘ofisi zake’ zilizopakwa rangi ya ACT

Comments

comments