Marekani imepeleka vikosi vingine vya wanajeshi zaidi ya 1,000 katika eneo la Mashariki ya Kati kufuatia taharuki iliyozuka kati yake na Iran.

Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Patrick Shanahan amesema kuwa uamuzi huo wa kupeleka vikosi ni kujibu kile alichokiita ‘tabia ya chuki’ ya majeshi ya Iran.

Jeshi la maji la Marekani pia limeweka hadharani taswira mpya zinazohusisha Iran na shambulizi la mabomba ya mafuta, Oman.

Jumatatu wiki hii, Iran ilitangaza kuwa haitazingatia tena sehemu ya makubaliano iliyosaini mwaka 2015 kuhusu Nyuklia baada ya kuona kuwa Marekani na washirika wake hawazingatii maeneo mengi ya makubaliano hayo.

Aidha, China imeisihi Iran kutoachana na mpango huyo wa makubaliano ya nyuklia wa mwaka 2015.

Marekani imeeleza kuwa inawapeleka wanajeshi wake kwa lengo la kulinda maslahi yake pamoja na watu wake.

“Mashambulizi ya hivi karibuni ya Iran yanathibitisha kuwa taarifa za kiintelijensia tulizokuwa tumezipata kuhusu tabia za chuki za majeshi ya Iran na washirika wake ni tishio kwa watu wa Marekani na maslahi yake katika eneo hilo,” amesema Shanahan.

Kikosi cha wanajeshi 1,000 waliopelekwa kimeongeza idadi kwa wanajeshi wengine 1,500 wa nyongeza ambao Rais Donald Trump aliwatangaza mwezi uliopita. Marekani ilikuwa na vikosi vyake tangu awali katika eneo hilo.

LIVE: Hafla ya kutambulisha tuzo ya 'SERENGETI' kuwa hifadhi bora barani Afrika
Video: Mgogoro wa ardhi wafikia pabaya, Wakili Manyama aingilia kati