Marekani imeishutumu vikali Urusi na kudai kuwa ndege za kivita za Urusi ndizo zilizohusika katika shambulio la  msafara wa magari ya kutoa misaada nchini Syria siku ya Jumatatu na kusababisha vifo.

Tuhuma hizo zimetolewa na Marekani dhidi ya Urusi baada ya ndege mbili za kivita za Urusi aina ya SU-24, kuonekana  angani, sambamba na msafara huo wa magari wakati tukio hilo likitokea.

Hata hivyo Urusi imekanusha na kusema kuwa ndege hizo hazikuwa zake wala za Syria, na kuongeza kuwa waasi ndio watakua wanahusika katika shambulio hilo.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema ndege zake zinazojiendesha zenyewe zilikuwa zikifuatilia msafara huo, lakini kamera zao zilijizima kabla ya shambulio hilo kuanza.

Shambulio hilo lilitokea siku ya Jumatatu lilifanyika  mara baada ya serikali ya Syria kutangaza kumaliza wiki ya kusitisha mapigano.

Tundu Lissu akwama Mahakamani, Dhamana yake hatarini
Kilimanjaro Queens Yawafuta Machozi Zanzibar Queens