Marekani imejitoa katika Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binaadamu na kulituhumu kuwa lina unafiki wa kisiasa wenye upendeleo.

Baraza hilo lililoundwa mwaka 2006, lenye makao makuu yake, Geneva limeshutumiwa kwa kuruhusu mataifa yenye rekodi mbaya yakutiliwa shaka ya haki za binaadamu kuwa wanachama.

“Taasisi hiyo niya kinafiki na upendeleo, inakejeli haki za binaadamu,” amesema mjumbe wa Marekani katika Umoja huo Nikki Haley

Aidha, wanaharakati wamesema kuwa hatua hiyo ya Marekani huenda ikaathiri jitihada za kuangalia na kushughulikia ukiukwaji wa haki za binaadamu kote duniani.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, katika taarifa iliyotolewa kupitia msemaji wake, amesema kuwa angependelea Marekani kubakia katika baraza hilo.

Hata hivyo, Kamishna wa haki za binaadamu katika Umoja wa mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein, ameitaja hatua hiyo ya kuwa ni yakusikitisha’ na kushangaza, wakati Israel, kwa upande wake imepongeza hatua hiyo ya Marekani

 

Pellegrini amrudisha Lukasz Fabianski ligi kuu
Mpina aomba radhi maofisa wake kupima samaki kwa rula