Marekani imeufungua rasmi ubalozi wake Jerusalem huku Wapalestina zaidi ya 40 wakiuawa na wengine wakijeruhiwa kwenye mapambano na askari wa Israel katika harakati za kuipinga hatua hiyo.

Hatua ya Marekani ya kuuhamishia rasmi ubalozi wake kwenye mji  wa Jerusalem kutoka Tel Aviv imetekelezwa baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Aidha, balozi wa Marekani nchini Israel, David Friedman amesema kuwa baada ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa taifa la Israel wakati muhimu kama huu ni wa kihistoria kwa sababu ya ujasiri wa mtu mmoja tu ambaye ni rais wa Marekani Donald Trump ameweza kuitambua Jerusalem.

Hata hivyo, Trump amesema kuwa Marekani itaendelea kujitolea kikamilifu katika kuuwezesha mpango wa amani wa Mashariki ya Kati.

Ali Kiba awafungukia wadukuzi wa YouTube, 'sijui wametumwa'
Video: Lulu azua mjadala nchini.., JWTZ yatakiwa isaidie Polisi kiintelijensia