Licha ya kushindwa kufikia malengo akiwa na kikosi cha Argentina wakati wa fainali za kombe la dunia 2018, na kupelekea mkataba wake kuvunjwa na chama cha soka nchini Argentina, kocha Jorge Sampaoli amegeuka lulu katika baadhi ya nchi za ukanda wa Amerika.

Sampaoli ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Chile wakati wa fainali za kombe la dunia 2014 na baadae klabu ya Sevilla ya Hispania anatajwa kuwa katika harakati za kupata ajira nyingine siku za karibuni.

Nchi za Marekani (USA), Costa Rica na Paraguay  zinatajwa kuwa katika mikakati ya kumgombea kocha huyo, kwa ajili ya kufanikisha mipango ya kuziwezesha timu  ao za taifa kufanya vyema kwenye michuano ya ukanda wa Amerika na kombe la dunia mwaka 2022.

Sampaoli, pia anahusishwa na mipango ya kunyatiwa na chama cha soka nchini Mexico ambacho kwa sasa kipo kwenye mchakato wa kumsaka kocha mpya, baada ya kuondoka kwa Juan Carlos Osorio.

Mfumo wa kocha huyo uliotumika wakati wa fainali za mataifa ya kusini mwa Amerika mwaka 2015 akiwa na timu ya taifa ya Chile, umekua moja ya sababu ambayo inamfanya kuwania na nchi hizo.

Katika mwaka huo Sampaoli aliwezesha Chile kutwaa ubingwa wa ukanda wa Amerika ya kusini kwa kuifunga Argentina kwa changamoto ya mikwaju ya Penati nne kwa moja katika mchezo wa fainali.

Waliojiuzulu Chadema wateuliwa CCM kugombea ubunge jimboni kwao
Mwakyembe ataka watanzania wanaolipishwa na StarTimes kupeleka ushahidi

Comments

comments