Marekani imeweka masharti kwa waombaji wa VISA wanaotaka kuingia nchini humo, kuwasilisha taarifa zao za mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuzikagua.

Kwa mujibu wa BBC, utaratibu mpya uliowekwa na Idara ya Marekani unamtaka muombaji kuwasilisha taarifa hizo za mitandao ya kijamii pamoja na majina ya barua pepe na namba za simu alizowahi kuzitumia katika kipindi kisichozidi miaka mitano.

Wakati wazo hilo lilipokuwa linafanyiwa kazi na Serikali ya Marekani mwaka jana, ilielezwa kuwa takribani watu milioni 14.7 wataathiriwa na zoezi hilo kila mwaka.

Utaratibu huo hautawahusu wanadiplomasia pamoja na wafanyakazi katika idara zinazohusika na utoaji VISA.

Imeelezwa kuwa tathmini na upembuzi utafanywa kwa kina zaidi kwa watu wanaotaka kuingia nchini Marekani kwa ajili ya masomo au kufanya kazi.

Athari za kiatu kirefu kwa mwanamke mjamzito
DC aeleza walivyomnasa mtuhumiwa kiongozi wa Teleza-Kigoma