Marekani na Korea Kusini zimeungana kwa pamoja kufanya mazoezi ya kijeshi ambayo hufanyika kila mwaka kwaajili ya kujiweka sawa na mashambulizi yeyote ambayo yanaweza kujitokeza.

Mazoezi hayo yamefanyika mara baada ya Korea Kaskazini kuendelea na mpango wake wa kufanya majaribio ya makombora ya nyuklia ya masafa marefu na kutishia kuishambulia Marekani.

Aidha, Korea Kaskazini imepinga vikali mazoezi hayo huku ikisema kuwa mazoezi hayo ni sawa na kumwaga petroli kwenye moto ambao ukilipuka kuuzima itakuwa ni ndoto.

China na Urusi zimependekeza kusitishwa kwa mazoezi ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kaskazini ili nayo Korea Kaskazini iache kuyafanyia majaribio makombora ya nyuklia ya masafa marefu.

Hata hivyo, Marekani imesema kuwa mazoezi hayo yatawahusisha wanajeshi 17,500 wa Marekani na Korea Kusini huku ikiongeza kuwa yatafanyika kwa muda wa siku kumi.

William Carvalho Akaribia Kutua London
Neymar Apandisha Mzuka Ufaransa