Mataifa ya Marekani (USA), Canada na Mexico yameshinda zabuni ya kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia mwaka 2026, huku wakiibwaga Morocco.

Mataifa hayo matatu yaliyoungana kwa pamoja, yametangazwa mshindi mchana huu baada ya wajumbe wa mkutano mkuu wa FIFA kupiga kura katika mkutano uliofanyika mjini Moscow nchini Urusi.

Mataifa hayo ya kaskazini mwa Amerika yamepata kura 134 kati ya kura 203 zilizopigwa, na Morocco imepata kura 65.

Hii inakua mara ya tano kwa taifa la Morocco kuwasilisha zabuni ya kuomba uenyeji wa fainali za kombe la dunia, na mara zote limeshindwa kufikia lengo la kuwa mwenyeji.

Fainali za kombe la dunia za 2026, zitaandika historia mpya ya kushirikisha mataifa 48, badala ya 32 yanayoshiriki sasa, kwa mujibu wa kanuni ya mashindano hayo.

Jumla ya michezo katika fainali za kombe la dunia kuanzia mwaka 2026 itakua 80 ambayo itachezwa katika miji itakayoteuliwa katika mataifa ya Marekani, Mexico na Canada.

Wasimamishwa kazi kwa kuisababishia hasara serikali
Real Madrid wamponza Julen Lopetegui