Klabu ya Lille italazimika kusubiri maamuzi ya Chelsea, baada ya kutuma ofa ya kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Michy Batshuayi Tunga.

Meneja wa Lille Marcelo Bielsa amedhamiria kumrejesha mshambuliaji huyo nchini Ufaransa, hata kwa usajili wa mkopo, baada ya kuona ana nafasi ya kufanya hivyo kutokana na Batshuayi kukosa wasaa wa kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha The Blues.

Dhamira kubwa ya Lille ni kutaka kumsajili moja kwa moja mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa ada ya Euro milioni 40, na kama itashindikana watalazimisha kumpata kwa njia ya mkopo.

Bielsa alibahatika kufanya kazi la Batshuayi alipokua Olympic Marseille, kabla ya kumruhusu kuondoka mwanzoni mwa msimu uliopita na kujiunga na Chelsea.

Heche awazodoa wasomi, asema uzalendo si kuiunga mkono Serikali
Lissu akamatwa na Jeshi la Polisi Dar