Kundi la Empire limesikitishwa na taarifa za awali ambazo zilitokea mapema mwezi Januari kuhusu muigizaji wa tamthilia ya Empire, Jussie Smollet ya ubaguzi wa rangi na jinsi alivyofanyiwa msanii huyo jijini Chicago.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ inaelezwa kuwa Jussie aliongea na mmoja wa rafiki zake anaefahamika kwa jina la Abel Osundairo siku nne kabla ya tukio hilo kutokea na alimuomba waonane huku akisisitiza kuwa anahitaji msaada wa kuongea naye, ingawa msanii huyo alikana meseji hizo kuhusika na tukio alilofanyiwa.

Inaelezwa kuwa kundi hilo limekasirika kutokana na Polisi kudhani kuwa Abel na Jussie walipanga mpango huo wa tukio la uvamizi ili ionekane ni kweli, taarifa zinadai kuwa Jussie alimpigia simu Abel kumjuza kuhusu ratiba ya mazoezi na si vinginevyo.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa uvamizi uliofanyika dhidi ya Jussie ni kweli na kesi kwa sasa bado ipo mikononi mwa Polisi na huku kundi la Empire likisikitishwa na vyombo vya habari kuripoti kuwa waliomfanyia ubaguzi Jussie ni watu wenye asili ya wazungu.

Iliripotiwa kuwa muigizaji huyo hata shiriki msimu mpya wa sitta wa tamthilia hiyo ya Empire kutokana na tuhuma zilizokuwa zikimkabili alipokuwa mjini Chicago.

Wananchi Wanging'ombe wajenga vyumba vya madarasa
JPM kuzindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi wilayani Chato

Comments

comments