Mapera ni miongoni mwa matunda ya msimu lakini yenye ladha nzuri na yanapotumiwa vizuri huweza kuwa na manufaa kadhaa ndani ya miili yetu, Husaiida kuimarisha kinga za miili kutokana na kuwa na vitamin C ya kutosha ndani yake.
Zifuatazo ni faida za Ulaji wa mapera katika mwili wa binadamu
Imelezwa kuwa mapera nu kinga nzuri ya kisukari, ulaji mbaya wa watu wengi unawaweka katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari lakini matumizi ya mapera yatakupunguzia hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari, hii ni kwa sababu mapera yana utajiri mkubwa sana wa Fibre ambayo ni muhimu katika kupunguza kiasi cha sukari kwenye damu.
Pia matumizi ya tunda hili humuweka mhusika kwenye uwezekano mdogo wa kukumbwa na matatizo ya saratani za aina mbalimbali.

Ulaji wa mapera pia husaidia kurekebisha kiwango cha shinikizo la damu Madini ya Potassium yaliyomo ndani ya mapera yanasaidia katika kupunguza shinikizo la damu ( Blood Pressure ) Ndizi na mapera vina kiwango cha potassium sawa.

Kuimarisha uwezo wa kuona, Mapera yana utajiri mkubwa sana wa Vitamin A au Retinol ambayo ni muhimu sana katika kusaidia kuona vizuri. Hivyo basi kama ilivyo kwa karoti, mapera yanasaidia sana katika kuongeza na kuimarisha uwezo wa mtu kuona.

Lakini pia Mapera ni muhimu katika afya ya akili ya mwanadamu vitamin B3, Vitamin B6 ambazo zinapatikana ndani ya tunda la mpera muhimu katika kuimarisha afya ya akili ya mwanadamu. Mapera yatasaidia kuufanya ubongo wako u ‘relax’.

Kenya: idadi ya waliothibitika kuwa na Corona yaongezeka
Uganda: Waliothibitika kuwa na virusi vya Corona wafikia 23