Timu ya Manchester United itamenyana na Paris Saint-Germain katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Timu nyingine tatu za England nazo zimepangiwa wapinzani wagumu kutoka Ujerumani katika hatua hiyo.

Liverpool imepangiwa Bayern Munich, wakati Manchester City itamenyana na Schalke na Tottenham Hotspur imepewa Borussia Dortmund.

Kikosi cha Jose Mourinho kinachosuasua kitaanzia nyumbani katika Uwanja wa Old Trafford kabla ya kusafiri kuwafuata matajiri wa Ufaransa kwa mchezo wa marudiano.

Man City, timu pekee ya England iliyoongoza kundi, itaanzia ugenini kabla ya kucheza nyumbani mechi ya marudiano, lakini timu nyingine zitaanzia ugenini.

Mechi za kwanza zitachezwa Februari 12, 13, 19 na 20 na za marudiano zitachezwa Machi 5, 6, 12 na 13 mwaka 2019.

Live: Rais Magufuli akihutubia katika maadhimisho ya kilele cha miaka 50 ya Bakwata
Mbunge alalamikia malipo kidogo ya Korosho

Comments

comments